Thursday, May 26, 2011
HAPPY BIRTHDAY MEL C
ACHENI HIIZOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
HII NI KWA WOTE WALE MA ADALAAAAAAAA,KAMA IMEKUGUSA IMEZE KIMYA KIMYA.
KWA NINI UNAVUA PETE YA NDOA??????????
hivi kwa nini baadhi ya wanandoa hawapendi kuvaa pete za ndoa,na hata wengine hudiriki kuzivua wanapokuwa na mambo yao hususan kazi za nje?????????????????.????????????
KUEPUKA HARUFU YA JASHO
Kwanza ni muhimu kujua nini kinasababisha mtu kunuka au kunukia.
Jasho linalotoka katika mwili wa mtu ni namna ya kupunguza joto la mwili, hili jasho ni mchanganyiko wa maji na kemikali za mwili ambazo zikikutana na bakteria husababisha harufu.
Jasho linalotoka katika mwili wa mtu ni namna ya kupunguza joto la mwili, hili jasho ni mchanganyiko wa maji na kemikali za mwili ambazo zikikutana na bakteria husababisha harufu.
Cha kufanya kuepuka hii harufu. Usafi wa hali ya juu yani kuoga mara kwa mara na vile vile matumizi ya pafyumu au bidhaa zinazotumika kupambana na jasho (antiperspirant) au kuondoa harufu ya jasho
(deodorant). Na matumizi haya yanapaswa kwenda sambamba na kazi au shughuli unazofanya.
Kama shughuli unazofanya zinahitaji nguvu na unatokwa na jasho sana basi unahitaji kuchagua bidhaa ambazo zitahimili mazingira yako ya kazi na kukuacha ukinukia vizuri wakati wote. Pia ni muhimu
kuzingatia suala la bei, tahadhari za matumizi na kudumu kwake.
Kudumu kwa pafyumu kunatokana na wingi wa mafuta kiujazo yani katika utengenezaji kuna kiwango cha mafuta ambacho kinatumika kuitengeneza. Wingi wa mafuta kwenye pafyumu kunasaidia mtumiaji.
kubaki ana nukia kwa muda mrefu “Eau de Perfumes (EDP) and Eau de Toilette (EDT).”
Kwa matumizi ya deodorant na antiperspirant, paka kwenye makwapa tu wakati unapohitajika kufanya hivyo hususan unapotoka kuoga.
Sehemu muhimu za kupaka pafyumu ili idumu kwa muda mrefu ni; nyuma ya masikio, shingoni, kwenye kiungio cha kuganja, nyuma ya kiwiko cha mkono na nyuma ya magoti. Kisha pulizia kidogo hewani kukuelekea wewe ili mwili wote uweze kuingiwa na unyevunyevu wa pafyumu
Na mwisho ni vizuri kupaka pafyumu unapotoka kuoga tu ila kuifanya idumu kwa muda mrefu, kwa wale wanaojifukiza kwa udi wanaelewa.
Na unashauriwa usipake pafyumu moja kwa moja kwenye makwapa kwa sababu inasababisha weusi na pia ina haribu nguo ikipakwa moja kwa moja kwenye nguo.
BREAKING NEWS...: VIONGOZI WA CHADEMA WATINGA MAHAKAMANI JIJINI ARUSHA LEO
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe, Katibu mkuu wa chama hicho Mh. Wilbroad Slaa na wabunge wa Moshi Mjini na Arusha mjini Mh. Philemon Ndesamburo na Goodluck Mrema wamefikishwa mahakama ya mkoa wa Arusha na kusomewa mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano.
Mchakato wa kuwawekea dhamana umefanikiwa
Mke wa Dk. Slaa, Josephine, akibubujikwa damu baada ya kujeruhiwa na askari polisi katika maandamano
Mchakato wa kuwawekea dhamana umefanikiwa
EPUKA UONGO KATIKA MAPENZI
Uongo ni sumu ya mapenzi.
Serikali imepiga marufuku uchimbaji wa kokoto eneo la Kunduchi, Barabara ya Bagamoyo, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kuwaonya watu wote wanaojihusisha na uchimbaji huo kuwa watachukuliwa hatua za kisheria
NDANI YA DUKA LA SHEAR ILLUSITION MILLENIUM TOWER
Grace Luhinda na Salma Dacotha
Tabia za kuepuka ili kuwa na ngozi nzuri
Mwanamke anafaa kuweka ngozi yake ivutie na kuwa nadhifu wakati wote. Kuna baadhi ya wanawake wanadhani kuwa nadhifu na kuvutia ni kupaka vipodozi vya aina mbalimbali na vya gharama, hapana, suala la muhimu zaidi ni kujua namna gani unaweza kuitunza ngozi yako ili ipendeze na kuwa yenye afya.
Kwanza kabisa unapaswa kuepuka msongo wa mawazo na hasira, wakati wote jaribu kuwa mtu mwenye furaha zaidi. Wataalam wanasema mikunjo inayoonekana kwenye nyuso za wanawake wengi, inasababishwa na wao kuwa wenye huzuni au kuwaza mambo mengi yanayopelekea kutoweka kwa furaha yao. Hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unaepuka vitu vinavyosababisha hasira katika maisha ya kila siku na kama ni ngumu kuepuka basi hakikisha hauviweki moyoni ili kudumisha furaha yako.
Pili, wanawake tumekuwa muda wetu mwingi tunautumia katika mihangaiko na tunasahau kupumzisha miili yetu vya kutosha. Ila ili uwe na ngozi yenye afya unapaswa kulala saa 6 mpaka 8 kwa siku ya saa 24, nikimaanisha ukilala saa 4 uamke saa 12 asubuhi na siyo mapema zaidi ya hapo.
Vyakula tunavyokula pia vinachangia uzuri wa ngozi yako, hivyo tunapaswa kuwa makini sana. Vya kuzingatia katika chakula chetu ni samaki na jamii ya vyakula vya baharini ambavyohusaidia kung’arisha na kulainisha ngozi, matunda haswa machungwa, machenza na maparachichi ni mazuri kwa kulainisha ngozi na kuifanya isiwe kavu, mbogamboga pia ni muhimu katika kutakasha ngozi hususan caroti, mboga za majani na viazi vitamu na mwisho ni nafaka zisizokobolewa kama vile mahindi, mtama au uyoga pia husaidia kuondoa madoa na mabaka kwenye ngozi.
Kama nilivyosema awali lishe ni muhimu sana katika kuimarisha ngozi yako, pia zingatia vinywaji unavyotumia, vilevi au pombe kali ni sumu kubwa ya ngozi kutokana na tabia ya kusababisha mwili kukaukiwa na maji wakati mwingi. Hivyo ukiwa mtumiaji wa vilevi hakikisha unakunywa maji mengi zaidi ya kawaida ili kufidia maji yanayopotea, na hata bila kutumia pombe maji ni muhimu sana katika kuboresha ngozi. Tumia lita moja na nusu hadi mbili kwa siku.Juisi ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu, husaidia kufanya ngozi yako kuwa nyororo na hata kuondoa mikunyanzi , matunda pia ni muhimu sanaaaaaaaa.
Usafi wa ngozi pia ni muhimu sana katika urembo, ngozi hususan ya uso ni muhimu kuoshwa mara mbili au tatu kwa siku yani asubuhi na jioni, kama ikiwekana mchana pia kulingana na aina ya ngozi yako na mahitaji yake. Tumia maji ya uvuguvugu kusafisha uso ila kuondoa uchafu na mafuta yasiyohitajika usoni, pia zingatia aina ya sabuni unayotumia iendanena ngozi yako, kama inawezekana nunua sabuni maalum kwa ajili ya uso.
Usiku kabla ya kwenda kulala hakikisha unapaka losheni maalum kwa ajili ya kutunza unyevu wa ngozi yako. Ukienda kwenye maduka ya dawa au vipodozi ulizia “moisturizer ya ngozi” ili kuhakikisha ngozi yako haikauki wala kukakamaa.
Na kwa wale wavutaji wa sigara, matokeo mazuri ya ngozi hayatapatikana isipokuwa kwa kuacha kuvuta sigara. Sumu inayotokana na sigara husababisha ngozi kusinyaa na kuzeeka, hivyo kufanya ngozi kupoteza mvuto wake.
Natumaini kwa leo umejifunza mambo mengi kuhusiana na ngozi pamoja na matunzo yake. Mambo muhimu ya kuzingatia ni lishe, usafi, muda wa kupumzika na pia kuepuka sigara, pombe na mawazo ya mara kwa mara.
Khadija Kopa alizwa
Pole bi Khadija Kopa kwa Maswahiba yaliyokukuta
Subscribe to:
Posts (Atom)